Grenfell Tower: Watu 79 wahofiwa kufariki mkasa wa moto London

Grenfell Tower Haki miliki ya picha Metropolitan Police
Image caption Picha mpya zinazoonesha hali ilivyo ndani ya vyumba vilivyokuwa makazi

Watu 79 wamefariki au hawajulikani walipo kufikia sasa kutokana na mkasa wa moto jumba la Grenfell Tower jijini London, polisi wamesema.

Kamanda wa polisi Stuart Cundy amesema hayo kupitia taarifa, na kuongeza kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Moto ulizuka katika jumba hilo la makazi la orofa 24 mtaa wa Kensington Kaskazini, magharibi mwa London mwendo wa saa saba usiku saa za London 14 Juni.

Familia nyingi zilipoteza zaidi ya jamaa mmoja, alisema Bw Cundy.

Miongoni mwa waliojeruhiwa, 18 bado wamelazwa hospitalini, tisa wakiwa hali mahututi.

Bw Cundy amesema kwa sasa wanapatia kipaumbele shughuli ya kuwatambua waliofariki ndani ya jengo hilo na kuondoa miili yao haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo, amesea si wote watakaoweza kutambuliwa na kwamba shughuli yenyewe ya kuwatambua watu wote waliofariki huenda ikachukua "wiki nyingi, nyingi sana".

Raia Uingereza walikaa kimya dakika moja saa tano mchana saa za huko kutoa heshima kwa wathiriwa.

Awali, polisi walitoa picha mpya za jumba hilo na kuonesha changamoto wanazokumbana nazo katika kujaribu kutafuta miili ya waliofariki.

Haki miliki ya picha Metropolitan Police
Image caption Picha ya polisi inayoonesha lango kuu la kuingia katika jumba hilo

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii