Mwandishi Walter Menya akamatwa na kuzuiliwa Kenya

Bw Menya (kulia) alitiwa mbaroni Jumapili
Image caption Bw Menya (kulia) alitiwa mbaroni Jumapili

Mwandishi wa gazeti moja la kibinafsi nchini Kenya atazuiliwa kwa siku moja zaidi baada ya kukamatwa Jumapili.

Mahakama imewaruhusu polisi kumzuilia Walter Menya kwa siku moja zaidi ili kukamilisha uchunguzi.

Polisi walikuwa wameomba waruhusiwe kumzuilia kwa siku tatu.

Bw Menya, anayefanyia kazi gazeti la Sunday Nation, anadaiwa kudai hongo ndipo aandike taarifa ya kumfaa mtu aliyetambulishwa kwa jina Kennedy Kiprotich Koros katika stakabadhi za mashtaka.

Polisi wanadai alipokea jumla ya $350 (£270) kupitia njia ya simu awali na kwamba alikamatwa alipoenda kupokea kiasi kingine cha $200.

Polisi walisema wanahitaji kupata ushahidi zaidi kutoka nyumbani kwa Bw Menya na katika afisi za shirika analofanyia kazi, shirika la Nation Media Group.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii