Champs Elysees: Gari la polisi lagongwa Paris

Paris, France, 19 Juni 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Afisa wa polisi akikimbia kuelekea kwenye gari hilo barabara ya Champs Élysées

Gari moja limeendeshwa makusudi na kugonga gari la polisi katika eneo la kifahari la Champs Élysées, katikati mwa Paris, maafisa wa polisi wamesema.

Gari hilo lilishika moto muda mfupi baadaye.

Dereva wa gari hilo amefariki.

Polisi wamepata bunduki aina ya Kalashnikov ndani ya gari hilo, bunduki nyingine kadha za kawaida na chupa zenye gesi.

"Maafisa wa usalama wamelengwa tena kwenye shambulio Ufaransa," waziri wa mambo ya ndani Gerard Collomb amesema, na kulitaja kuwa "jaribio la shambulizi".

Hakuna raia au maafisa wa usalama waliojeruhiwa.

Ufaransa kwa sasa imo katika hali ya hatari baada ya kutokea kwa msururu wa mashambulio miaka ya akribuni.

Polisi aliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili wakajeruhiwa katika shambulio Champs Élysées Aprili, siku chache kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Kisa cha sasa kimetokea siku moja baada ya uchaguzi wa ubunge nchini Ufaransa, ambapo chama cha Rais Emmanuel Macron kilipata ushindi mkubwa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maafisa wa kutegua mabomu wakikagua gari lililogongeshwa kwenye gari la polisi
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Foleni ya magari iliyosababishwa na operesheni ya kiusalama eneo hilo
Haki miliki ya picha AFP

Mada zinazohusiana