Wanasayansi wavumbua chanjo ya magonjwa ya moyo

Netherland
Image caption Mfano wa chanjo hiyo

Shirika la utafiti wa kisayansi kutoka nchini Netherlands limeanza kufanya majaribio kwa wanadamu ya chanjo ya kupunguza kiwango cha mafuta katika mwili wa mwanaadamu na kwamba endapo utafiti huo utafanikiwa; wana matumaini kuwa chanjo hiyo itakuwa na uwezo wa kuzuia magonjwa ya moyo.

Watafiti hao wameeleza kuwa majaribio yao waliyokwisha kuyafanya dhidi ya panya yanaonesha kwamba chanjo hiyo imefanikiwa kuzuia na kuacha kuimarisha amana ya mafuta katika mishipa ya damu.

Imearifiwa kuwa chanjo hiyo ina uwezo wa kufanya mfumo wa kinga ya mwili kukabiliana na mafuta yasiyohitajika kutoka katika damu.

Image caption Je watu wenye miili mikubwa wamepata ukombozi?

Wanasayansi hao wanaamini kuwa chanjo hiyo inaweza kutumika kama njia mbadala wa zilizokuwa za kupunguza mafuta , pamoja na kuwasaidia, mamilioni ya watu ulimwenguni kupambana na mafuta yasiyohitajika mwilini.

Inatarajiwa kuchukua takriban miaka sita ili vipimo hivyo kukamilika.

Mada zinazohusiana