Iran yakana watu waliokamatwa na Saudia ni wanajeshi wake

Rais wa Iran Hassan Rouhani: Iran imekana watu waliokamatwa na Saudia ni wanajeshi wake
Image caption Rais wa Iran Hassan Rouhani: Iran imekana watu waliokamatwa na Saudia ni wanajeshi wake

Iran inasema kuwa watu watatu waliokamatwa na wanamaji wa Saudia siku ya Ijumaa ni wavuvi na wala sio wanajeshi wake.

Mkuu wa maswala ya mipakani katika wizara ya maswala ya ndani nchini humo Majid Aghababaie alisema kuwa utambulisho wa unajulikana na kwamba na kwamba hakuna ushahidi kwamba walikuwa wanajeshi.

Saudia iliwakamata wakati boti yao ilipokuwa ikiwasili karibu na ufukwe mmoja wa bahari ulio na mafuta na kusema kuwa ni wanachama wa jeshi la Iran.

Kitengo cha habari cha Saudia kilitangaza kuwa shambulio la kigaidi katika eneo hilo la mafuta limetibuliwa.

Mada zinazohusiana