Wasiwasi wazidi Ureno kuhusu kuzuka kwa mioto

Wasiwasi wazidi Ureno kuhusu kuzuka kwa mioto Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wasiwasi wazidi Ureno kuhusu kuzuka kwa mioto

Kuna wasi wasi mkubwa nchini Ureno kuwa viwango vya juu vya joto vinavyoendelea kushuhudiwa nchini humo, huenda vikaanzisha upya mioto katika misitu nchini humo, ambayo tayari imesababisha vifo vya watu sitini na wanne, katika eneo la Pedrogao Grande, Kaskazini mwa mji mkuu wa Lisbon.

Utawala wa nchi hiyo unasema kuwa asilimia sabini ya moto huo sasa umethibitiwa, lakini wasiwasi wao ni viwango vya joto na upepo mkali unaoendelea kushuhudiwa.

Zaidi ya wazima moto wanaendelea kupambana kuuzima moto huo.

Vijiji kadhaa vimeteketezwa kabisa.

Watu wengi walikufa ndani ya magari yao au wakati walipokuwa wakijaribu kukimbia.

Zaidi ya watu mia moja thelathini wamejeruhiwa.