Brexit: Uingereza yakubali kuondoka kwa awamu

Wajumbe wa Uingereza na Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya BREXIT Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wajumbe wa Uingereza na Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya BREXIT

Baada ya siku ya kwanza na mazungumzo, mjini Brussels Ubelgiji, Uingereza imekubali mpango wa Muungano wa Ulaya wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo kwa hatua.

Waziri wa Uingereza anayeongoza mpango huo David Davis, amekubali kusitisha mazungumzo kuhusu mikataba ya kibiashara kati ya pande hizo mbili hadi hatma ya raia wa pande hizo walioko mataifa ya EU na fidia ya mwisho ya utengano kuafikiwa.

Aidha amesema ni wazi kwamba pande zote mbili zinataka kupata kustakabali mzuri wa uhusiano wao.

Naye Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo hayo Michel Barnier amesema kwa pande zote mbili Umoja wa Ulaya na Uingereza makubaliano ya haki yanawezekana na ni bora zaidi kuliko kutofanya kabisa.

Mada zinazohusiana