Zaidi ya watu 3000 wameuwawa DRC tangu Oktoba

Mapigano yamekuwa kati ya wanajeshi na kundi la waasi lakini pia raia wamejipata ndani ya mapigano hayo. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano yamekuwa kati ya wanajeshi na kundi la waasi lakini pia raia wamejipata ndani ya mapigano hayo.

Kanisa katoliki nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, limesema kuwa watu 3,383 wameuawa kwenye ghasia nchini humo katika eneo la Kasai tangu mwezi Oktoba, kwa mujibu wa Reuters.

Reuters linasema idadi hiyo inatokana na ripoti kutoka kwa kanisa.

Umoja wa Mataifa uliripoti kugunduliwa kwa zaidi ya makaburi 20 makubwa ya pamoja lakini uliweka viwango vyake kuwa watu 400.

Mapigano yamekuwa kati ya wanajeshi na kundi la waasi lakini pia raia wamejipata ndani ya mapigano hayo.

Reuters inasema kuwa kanisa limepata kuwa jeshi liliharibu vijiji 10.

Katika ripoti tofauti baraza la wakimbizi la Norway lilisema kuwa zaidi ya watu 1.3 wamehama makwao kutoka na ghasia hizo, katika kile linataja kuwa moja na majanga makubwa zaidi ya kuhama watu duniani. leo hii.

Mada zinazohusiana