Wanafunzi wa shule ya msingi wawapiga walimu Kenya

Wanafunzi wawatandika walimu Kenya
Image caption Wanafunzi wawatandika walimu Kenya

Shule moja nchini Kenya imefungwa baada ya wanafunzi kuwavamia na kuwapiga walimu, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la nchi hiyo.

Gazeti hilo linasema kuwa wanafunzi hao walionekana wakiwa na rungu na viboko wakiwavamia walimu wa kike ambapo walimu watatu walipata majeraha mabaya.

Baadaye polisi walifika katika shule ya msingi ya Kirimon na kufyatua risasi hewani.

Televisheni ya NTV nchini Kenya, ilisema kuwa wanafunzi walikuwa wakilalamikia adhabu ambayo walipewa.

Waakilishi kutoka chama cha walimu walisema shule hiyo itafungwa hadi Ijumaa wakati mkutano kati ya walimu, wazazi na wizara ya elimu utafanyika.