Atupwa jela kwa kuyumbisha mtoto kutoka jengo refu

Atupwa jela kwa kuyumbisha mtoto kutoka jengo refu Haki miliki ya picha Al Arabia
Image caption Atupwa jela kwa kuyumbisha mtoto kutoka jengo refu

Mwananamume mmoja nchini Algeria amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela, baada ya kuyumbisha mtoto kutoka kwa dirisha la jengo refu ili kuvutia wafuasi 1000 katika akaunti yake ya Facebook.

Mwanamume huyo alichapisha picha yake akimshika mtoto wake nje ya dirisha akiwa ameandika, "wafuasi 1000 au nimuangushe mtoto,"

Picha hiyo ilisababisha watumiaji wengi wa mtandao kushinikiza achukuliwe hatua za kisheria kwa kumdhulumu mtoto.

Mada zinazohusiana