Australia yasitisha mashambulizi Syria

An F/A-18E Super Hornet (similar to the one pictured) shot down the Syrian plane Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege ya F/A-18E Super Hornet sawa na iliyoshambuliwa na Marekani

Australia inasema kuwa inasitisha kwa muda oparesheni zake za kijeshi nchini Syia baada ya onyo kutoka Urusi kuwa italenga ndege za muungano unaoongozwa na Marekani,

Serikali ya Australia inasema kuwa hatua hiyo ni ya kuchukua tahadhari.

Onyo hilo la Urusi linakuja baada ya Marekani kuiangusha ndege ya jeshi la Syria.

Urusi pia ilisema kuwa imesitisha mawasiliano Marekani kwa lengo la kuzuia visa kama hivyo.

Australia imepeleka karibu wanajeshi 780 kama sehemu ya muungano unaoongozwa na Marekani kupigana na kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Marekani linasema ndege hiyo ilikuwa ikishambulia wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani katika mji wa Tabqa mkoa wa Raqqa.

Australia ina kikosi kidogo lakini chenye uwezo cha ndege sita zaF/A-18, manuwari ya kivita na ndege ya kutoa tahadhari, vyote vilivyo huko Al Mainhad milki ya nchi za kiarabu.

Masmbualia mengie ya Australia yemfanywa nnchini Iraq licha ya ndme zake poia kuhudumua nchini Syria.

Austalia imechukua hatua hiyo baada ya Marekani kuiangusha ndege ya Syria ambayo, ambayo jeshi la Marekani linasema kuwa ilikuwa ikishambulia wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani katika mji wa Tabqa mkoa wa Raqqa.

Lilitajwa kuwa shambulizi la kwanza la ndege moja hadi nyinginr kuwai kufanywa na Marekani tangu vita vya Kosovo mwaka 1999.