Joto lasababisha safari za ndege kufutwa Marekani

A plane is silhouetted against the sky as it takes off from Heathrow Airport 19 December 2002 in London, England. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shirika la American Airlines, lilitangaza kuwa lilikuwa likifuta safari kadhaa zilizokuwa zitoke uwanja wa Sky Harbor.

Huku joto likizidi kupanda katika mji wa Phoenix jimbo la Arizona nchini Marekani, zaidi ya safari za ndege 40 zimefutwa kwa sababu joto ni jingi kwa ndege kuruka.

Utabiri wa hali ya hewa katika mji huo unasema kuwa viwango vya joto katika mji huo vinaweza kufika nyuzi joto 120F au 49C siku ya Jumanne.

Hivyo ni viwango vya juu zaidi kwa ndege zingine kuweza kuruka.

Shirika la American Airlines, lilitangaza kuwa lilikuwa likifuta safari kadhaa zilizokuwa zitoke uwanja wa Sky Harbor.

Taarifa kutoka Phoenix zilisema kuwa hatua hiyo iliathiri ndege ndogo ambazo viwango vya juu zaidi kuhudumu ni nyuzi 118F au 48C.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Taarifa kutoka Phoenix zilisema kuwa hatua hiyo iliathiri ndege ndogo ambazo viwango vya juu zaidi kuhudumu ni nyuzi 118F au 48C.

Wakati wa viwango vya juu vya joto, hewa huwa nyepesi hatua ambayo husababisha kuwepo ugumu wa ndege kupaa kuenda mbali.

Kufuatia hilo ina maana kuwa ndege itahitaji nguvu nyingi zaidi kuweza kupaa angani.

Ndege kubwa kama ya Boeng 747 na Airbus zina uwezo wa kuhudumu katika viwango vya juu vya joto na hivyo hazijaathiriwa na viwango vya joto huko Phoenix.