Shambulio la bomu Brussels, mtuhumiwa auawa

Polisi katika eneo la tukio Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi katika eneo la tukio

Wanajeshi wa Ubelgiji wamemuua kwa kumpiga risasi mlipuaji wa bomu wa kujitoa muhanga, katika kituo kikuu cha reli mjini Brussels.

Idara ya polisi imesema kuwa mtu huyo alikuwa amevalia kile kilichoonekana kuwa mkanda wa vilipuzi na kuwa kulitokea mlipuko mdogo.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa mshukiwa huyo amefariki.

Watu waliokuwa katika kituo Kikuu cha mabasi mjini Brussels na eneo la karibu la mnara ambalo hufurika watalii wote waliondolewa.

Wanajeshi wamekuwa wakilinda doria mjini Brussels tangu mwaka uliopita kulipotokea shambulio la kujitoa mhanga katika eneo la Uwanja wa ndege na kwenye mfumo wa usafiri wa chini ya ardhi.