Rais Nicholas Maduro afanyia jeshi mabadiliko

Majeshi ya Venezuela yadaiwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya raia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majeshi ya Venezuela yadaiwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya raia

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amewabadili makamanda wanne wa ngazi za juu wa jeshi la nchi hiyo, kutokana na tuhuma kwamba majeshi ya ulinzi yamekuwa yakitumia risasi za moto wakati wa maandamano kwenye ghasia zilizozuka nchini humo kwa miezi kadhaa.

Jumla ya watu 75 wamefariki dunia toka kuanza kwa mwezi April.

Siku ya Jumatatu kulitolewa maoni makali wakati kipande kipya cha video kilipokuwa kikionesha wanajeshi watatu wa kikosi cha ulinzi wakionekana wazi wakiwashambulia kwa risasi waandamanaji.

Mmoja wao tayari amekamatwa.

Rais Maduro pia ametangaza uandikishaji wa polisi wapya elfu arobaini na walinzi wa taifa.