Wagombea wa Trump washinda uchaguzi Marekani

Bi Karen Handel wa Democrat akifurahia ushindi wake Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bi Karen Handel wa Democrat akifurahia ushindi wake

Chama cha Republican kimeshinda uchaguzi muhimu wa bunge la Congress katika jimbo la Georgia ulioonekana na wengi kuwa kura ya maoni dhidi ya utawala wa rais Donald Trump.

Huku kura zote ikiwa zimehesabiwa, mgombea wa Republican Karen Handel alishinda kwa asilimia 53 huku mgombea wa Democrat akijipatia asilimia 47.

Katika Jimbo la Carolina Kusini, mgombea wa Republican Ralph Norman alimshinda mgombea wa Democrat Archie Parnell katika ngome ya wahafidhina.

Spika wa bunge Paul Ryan alimpongeza Bi Handel kwa ushindi huo mgumu.

Chama cha Democrat kilishindwa kwa kura chache katika maeneo ya Kansas na Montana mwaka huu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mgombea wa Republican Jon Ossoff baada ya ushindi wake

Katika jimbo la Georgia matumizi ya uchaguzi huo yalifikia dola milioni 56 ikiwa ndio uchaguzi uliogharamikiwa katika historia ya Marekani.

Bwana Ossoff alishindwa kupata asilimia 50 ya kura zilizohitajika ili kuibuka mshindi katika uchaguzi wa jimbo la Atlanta mnamo mwezi Aprili, hivyobasi kulazimisha awamu ya pili ya uchaguzi dhidi ya Handel.

Democrats walitumai kutumia fursa ya kushuka kwa umaarufu wa Trump kushinda kiti cha Georgia.