Ndege ya kijeshi ya Urusi yaitishia ile ya Marekani Baltic

Ndege ya Marekani ya ujasusi aina ya US RC-135 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege ya Marekani ya ujasusi aina ya US RC-135

Ndege ya Urusi ilipaa futi tano juu ya ndege ya ujasusi ya Marekani katika anga ya bahari ya Baltic siku ya Jumatatu, kulingana na maafisa wa Marekani.

Hatua hiyo ilionekana kuwa isio salama kutokana na kasi ya ndege hizo mbali na udhibiti mbaya wa ndege hiyo, maafisa hao walisema.

Lakini Urusi imepinga malalamishi hayo ya Marekani ikisema kuwa ndege hiyo ya Marekani iliichokoza ndege yake.

Siku ya Jumatatu Urusi iliionya Marekani kwamba ndege za Marekani zinazopaa juu ya anga ya Syria zitalengwa.tangazo hilo lilijiri ili kujibu kuangushwa kwa ndege ya Syria baada ya kulenga waasi wanaoungwa mkono na Marekani.

Siku ya Jumanne, Jeshi la Marekani liliiangusha ndege isiokuwa na rubani inayomilikiwa na Iran nchini Syria na hivyobasi kuongeza wasiwasi kati ya Washington na Moscow ambayo ni mshirika mkuu wa utawala wa Syria.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege ya Ursui aina ya Su-27 ilipaa futi tano juu ya ndege ya Marekani

Uchokozi huo wa siku ya Jumatatu ulifanyika kilomita 40 kutoka eneo la Urusi la Kalinigrad katika maji ya kimataifa.

Msemaji wa Pentagon Nahodha Jeff David aliambia maripota kwamba:Tulikuwa tukipaa katika maji ya kimataifa na hatukufanya uchokozi wowote.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii