Mfalme wa Saudia amfuta kazi mrithi wake

Mfalme Salman wa Saudia amemfuta kazi mrithi wake
Image caption Mfalme Salman wa Saudia amemfuta kazi mrithi wake

Mfalme Salman wa Saudia amebadilisha mkondo wa urithi na kumfanya mwanawe wa kiume Mohammed bin Salman kuwa mwanamfalme na kuwa wa kwanza kumrithi.

Aliyekuwa mwanamfalme Mohammed bin Nayef amepokonywa taji lake na kufutwa kazi kama waziri wa maswala ya ndani.

Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31 ataendelea kuwa waziri wa ulinzi mbali na kuwa naibu waziri mkuu.

Mabadiliko hayo yalitangazwa katika misururu ya amri za kifalme.

Chombo cha habari cha Saudia kimesema kuwa mfalme ametaka raia wa taifa hilo kumtii mwanamfalme huyo mpya siku ya Jumatano.

Hatua ya kumpa cheo hicho Salman iliidhinishhwa na wanachama 31 kati ya 34 wa baraza kuu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mohammed Salman kushotoachukua mahala pake Mohammed Nayef

Wadadisi wanasema kuwa wale walio madarakani hupenda kuwateua watoto wao wa kiume kwa nafasi ambazo zitawawezesha kupandishwa vyeo.

Mfalme Salman ambaye ni mtoto wa Mfalme Abdulaziz alishika hatamu za uongozi mwaka 2015 baada ya kifo cha ndugu wa kambo Abdullah bin Abdul Aziz.

Alifanya mabadiliko makubwa kwa baraza lake la mawaziri miezi michache baadaye na kumpandisha cheo Mahammed bin Nayef kuwa mrithi na Mohammed bin Salam ambao wakati huo hawakuwa na umaarufu.