Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Uber ajiuzulu

Mkurugenzi mkuu wa kjampuni ya Uber Travis Kalanick ajiuzulu Haki miliki ya picha ERIC PIERMONT/AFP/GETTY
Image caption Mkurugenzi mkuu wa kjampuni ya Uber Travis Kalanick ajiuzulu

Travis Kalanick mkurugenzi mkuu wa kampuni ya uchukuzi ya Uber amejiuzulu kufuatia shinikizo kutoka kwa wawekezaji watano wakuu.

Kulingana na gazeti la New York Times hatahivyo atasalia katika bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo.

Wiki iliopita alisema kuwa anachukua likizo na hatakuwepo.

Hii inafuatia kujiuzulu katika bodi tajiri na mwekezaji David Bonderman.

Alijiuzulu baada ya kutoa tamko la kukandamizi jinsia katika mkutano wa kampuni hiyo.

Uber imekuwa ikikabiliana na madai ya unyanyasaji, ubaguzi na ukosefu wa nidhamu katika kazi.