Jaji afungwa kwa kukaidi agizo la mahakama India

Jaji afungwa kwa kukaidi agizo la mahakama Haki miliki ya picha PRESS TRUST OF INDIA
Image caption Jaji afungwa kwa kukaidi agizo la mahakama

Jaji mmoja nchini India ambaye amekuwa mafichoni tangu ahukumiwe kifungo jela amekamatwa na kufungwa.

Jaji CS Karnan alikuwa jaji wa kwanza wa mahakama kuu nchini India kukabiliwa na kifungo.

Alikamatwa katika jimbo la kusini la India Tamil Nadu siku ya Jumanne usiku.

Alihukumiwa kifungo mjini Kolkata huku ombi lake la kumwachilia kwa dhamana siku ya Jumatano likikataliwa na mahakamu ya juu zaidi .

Jaji huyo wa zamani alipatikana na hatia ya kutoa madai dhidi ya majaji wenzake.

Alihukumiwa kwa kukaidi agizi la mahakama na mahakama ya juu zaidi baada ya kutuma barua kwa waziri mkuu Narendra Modi ambapo alimtaka kuwachukulia hatua majaji wenzake.

Alipokonywa nguvu zake kama jaji mnamo mwezi Februari.