Walimu wapewa bunduki Colorado, Marekani

A man shoots at a target at a shooting range during a class to qualify for a concealed carry permit, 14 February 2014 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Walimu wapewa bunduki Colorado, Marekani

Walimu wanapewa mafunzo ya kubeba bunduki wakiwa shuleni katika jimbo la Colorado nchini Marekani ili kuwalinda watoto kama hatua baada ya mauaji ya watoto mwaka 2012.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanayohusu bunduki na ya kutoa matibabu yalianza siku ya Jumanne katika kaunti ya Weld..

Watu 17 ambao watapewa bunduki hizo tayari wameshiriki mafunzo hayo.

Mpango huo ni wa kuruhusu watu wa kujitolea kuingia shuleni wakiwa na bunduki chini ya sheria ya Marekani ya kubeba bunduki.

Walimu walipelekwa kwa majiribio ya kupiga risasi karibu na Denver ambapo walijaribiwa uwezo wao wa kutumi bunduki.

Lakini hatua hiyo imekasirisha makundi kama ya Safe Campus Colorado, ambayo yanawashauri wafuasi kushinikiza mamlaka kusaidia kuondoa bunduki shuleni

Mada zinazohusiana