Mahakama ya Misri yazuia kusalimishwa visiwa kwa Saudi Arabia

Mahaka ya Misri yazuia kusalimishwa visiwa vya Saudi Arabia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mahaka ya Misri yazuia kusalimishwa visiwa vya Saudi Arabia

Mahakama ya juu nchini Misri imesitisha kwa muda hatua ya kusalimisha visiwa viwili katika bahari ya shamu kwa Saudi Arabia hadi pale itakapo amua ikiwa makabaliano hayo yanaambatana na katiba.

Uamuzi huo wa mahakama ya juu ya katiba unakuja wiki moja baada ya bunge kuidhinisha makubaliano hayo ambayo yamepingwa na wamisri wengi.

Makakama moja tayari imepinga uamuzi huo ambao bunge linasema kuwa uko chini ya idhini yake.

Serikali ya Misri inasema visiwa hivyo viwili vinavyoitwa Tiran na Sanafir, vinamilikiwa na Saudi Arabia lakini lvilikodishwa kwa Msiri miaka 1950.

Mada zinazohusiana