Wanyama wakubwa wa porini waongezeka Kenya kwa asilimia 72

Shirika la wanyamapori nchini Kenya linasema kuwa idadi ya ndovu, nyati na twiga imeongezeka kwa asilimia 72 tangu mwaka 2014 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shirika la wanyamapori nchini Kenya linasema kuwa idadi ya ndovu, nyati na twiga imeongezeka kwa asilimia 72 tangu mwaka 2014

Mamlaka za kusimamia sekta ya wanyamapori nchini Kenya inasema kuwa idadi ya wanyamapori walio kwenye hatari ya kuangamia imeongezeka nchini humo.

Miaka ya hivi karibu, Kenya imekuwa ikikumbwa na uwindaji mkubwa wa wanyamapori.

Shirika la wanyamapori nchini Kenya KWS linasema kuwa idadi ya ndovu, nyati na twiga imeongezeka kwa asilimia 72 tangu mwaka 2014 wakati shughuli ya mwisho ya kuhesabu wanyama hao ilifanyika.

Kenya ilikumbwa na visa vya uwindaji mwaka 2012 na 2013 vilivyosababisha kuuawawa kwa ndovu wengi pamoja na faru kuliko wakati wowote katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Katika hatua za kukabiliana na suala hilo seriki ilitangaza sheria mpya ya hata kifungo cha maisha kwa muwindaji.

Lakini licha ya hilo uwindaji haramu pamoja na mizozo kati ya binadamu na wanyamapori vimesalia changomoto nchini Kenya.

Mada zinazohusiana