Uchaguzi Marekani 2016: Urusi yadaiwa kudukua majimbo 21

Raia wa Marekani wakishiriki katika shughuli ya upigaji kura 2016 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia wa Marekani wakishiriki katika shughuli ya upigaji kura 2016

Wadukuzi wa Urusi walilenga majimbo 21 wakati wa kampeni za uchaguzi wa Marekani ,kulingaa na maafisa wa Marekani.

Jeanette Manfra wa idara ya usalama wa ndani alikataa kutaja majimbo hayo wakati alipokuwa akitoa ushuhuda wake mbele ya jopo la seneti akidai kulikuwa na makubaliano ya siri.

Lakini aliongezea kwamba kulikuwa hakuna ushahidi kuonyesha kwamba masunduku ya kupigia kura yaliingiliwa wakati huo wa udukuzi.

Vitengo vya kijasusi vya Marekani vinaamini kwamba Moscow iliingilia kati uchaguzi huo ili kumsaidia Donald Trump kuibuka mshindi.

Bi Mafraambaye ni kaimu naibu wa maswala ya usalama wa mitandao ,alitoa ushahidi wake siku ya Jumatano mbele ya kamati ya seneti inayosimamia maswala ya ujasusi ambayo inachunguza madai ya Urusi kuingilia kati uchaguzi huo wa 2016.

Kufikia sasa tuna ushahidi kwamba mifumo ya uchaguzi katika majimbo 21 ililengwa,aliambia jopo hilo.

Alisema kuwa idara yake bado ina matumaini kuhusu mfumo wa uchaguzi wa Marekani ambao ni ''imara kimsingi''.

Urusi kwa mra nyengine imekana kuhusishwa na udukuzi wa uchaguzi wa Marekani huku rais Trump akifutilia mbali madai kwamba kampeni yake ilishirikiana na Urusi kama ''habari bandia''.