Manchester City yamwinda Dani Alves

Beki wa upande wa kulia wa Juventus Dani Alves kuelekea Manchester City Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa upande wa kulia wa Juventus Dani Alves kuelekea Manchester City

Juventus imethibitisha kwamba itamwachilia huru beki wa kulia Dani Alves katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake.

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amedaiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye walijuana naye tangu akiwa mkufunzi wa Barcelona.

Akizungumza kwa vyombo vya habari vya Italy siku ya Jumatano, afisa mkuu wa klabu hiyo Beppe Marotta amesema kuwa Alvez amekuwa na hamu kucheza katika klabu nyengine.

Marotta amesema kuwa Juventus inatumai kuafikiana kuhusu kandarasi yake na Alves.

Amemtakia maisha mazuri mchezaji huyo.

Alves amekuwa na Juve kwa mwaka mmoja , baada ya kushinda na Serie A mbali na kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

kabla ya kujiunga na klabu hiyo alikuwa ameichezea barcelona kwa kipindi cha miaka minane.

Misimu mitatu kati yazo ilikuwa chini ya ukufunzi wa Guardiola, kipindi ambacho wawili hao walijishindia mataji mawili ya kilabu bingwa, mbali na kombe la La Liga mara tatu.