Qatar yaomba kununua asilimia 10 ya shirika la ndege la American Airlines

American Airlines aircraft Haki miliki ya picha AFP
Image caption Qatar yaomba kununua asilimia 10 ya shirika la ndege la American Airlines

Shirika la ndege la American Airlines limepata ombi kutoka shirika la Qatar Airlines ambalo linataka kununua asilimia 10 ya shirika hilo la Marekani.

American Airlines ilisema kuwa Qatar ina nia ya kununua dola milioni 808 ya hisa zake.

Hisa kwenye shirika la American Airlines ambalo ndilo kubwa zaidi duniani zilipanda kwa asilimia 3.5 mwanzo wa mauzo.

Mwaka 2015 Qatar Airways ilinunua asilimia 10 katika kampuni ya International Airlines Group (IAG) ambayo ni mmiliki wa British Airways na Iberia.

Baadaye mwaka 2015 iliongeza hisa zake hadi asilimia 20 na kuwa mmiliki wa hisa nyingi zaidi huko IAG.

Mapema mwezi huu Saudi Arabia, Misri, Bahrain na milki ya nchi za kiarabu, Libya, Yemen na Maldive, walikata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar.

Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri zote zilisema kuwa zitasitisha safari za ndege kutoka Qatar na kufunga anga zake kutoka kwa ndege za nchi hiyo.