Genge la kijihad lavunjwa Morocco

Morocco Haki miliki ya picha Google
Image caption Moja wapo ya pwani za nchini Morocco

Maofisa wa serikali nchini Morocco wamearifu kwamba wamevunja gereza moja la watuhumiwa wanaodhaniwa kuwa wakijeshi ambalo lilikuwa na ukaribu na wanamgambo wa dola ya kiislam ambao walikuwa wana panga mipango ya mashambulizi makubwa.

Maofisa hao wamearifu kuwa watu wanne wanaoshukiwa kujihusisha na njama hizo wamekamatwa na silaha zao zinashikiliwa wakati wa oparesheni iliyoendeshwa Katika mji wa mapumziko wa pwani ya Essaouira.

Inaaminika kuwa jela hiyo imekuwa ikitekeleza matukio yake kwa kulenga maeneo ya kitalii katika pwani hiyo.