Mwandani wa aliyekuwa rais wa K. Kusini afungwa jela

Mwandani wa aliyekuwa rais wa K. Kusini Park Geun Hye ,Choi Soon-sil afungwa jela Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwandani wa aliyekuwa rais wa K. Kusini Park Geun Hye ,Choi Soon-sil afungwa jela

Mwandani wa aliyekuwa rais wa Korea Kusini amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya ufisadi.

Kushtakiwa kwa Choi Soon-sil ambako ni kwa kwanza baada ya kuomba zabuni kwa niaba ya mwanawe ni miongoni mwa kashfa zilizosababisha kuangushwa kwa utawala wa rais Park Geun hye.

Alifanya kazi kwa miaka minne kama mshauri wa bi Park ambaye alihojiwa na baadaye kushtakiwa.

Choi pia anakabiliwa na mashtaka kwamba alikubali hongo kutoka kwa Park.

Bi Park amekana madai yote ya ufisadi.

Choi alipatikana na hatia ya kutumia wadhfa wake kushawishi maafisa wa chuo kikuu kumuingiza katika shule hiyo mwanawe wa kike, mbali na kumpatia alama za mitihani ambayo hakufanya.

Mahakama ilisema katika uamuzi wake kwamba alifanya makosa mengi kuonyesha kuwa vitendo vyake vilikuwa upendo wa mama ambaye alitaka mwanawe kufanikiwa kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.

Maafisa wawili wa zamani katika chuo kikuu cha Ewha Womens University mjini Seoul pia wamefungwa kwa kushirikiana na Choi.

Choi pia anakabiliwa mashtaka mengine ikiwemo kutumia vibaya mamlaka, kulazimisha, kujaribu kulazimisha na kujaribu kufanya udanganyifu.

Waendesha mashtaka wanasema mwanawe bi Chung alihusika na uhalifu wa kiuchumi, udanganyifu katika mitihani, kuzuia biashara na kuficha kesi ya jinai.