Muigizaji azungumza kuhusu ''mauaji'' ya Trump

Muigizaji wa Caribbean Haki miliki ya picha EPA
Image caption Muigizaji wa Caribbean

Muigizaji wa filamu Johny Depp alitishia kumuua rais wa Marekani Donald Trump wakati wa hotuba katika sherehe za Glastonbury.

Je unaweza kumleta Trump hapa? Aliwauliza mashabiki huku akizindua filamu yake ya The Libertine.

Baada ya kuzomwa na mashabiki aliongezea: Hamukuelewa kabisa ni lini muigizaji alimuua rais? Nataka kuweka wazi ,aliongezea.

''Mimi ni muigizaji. Ninadanganya ili kulipwa. ni kitambo nadhani ni wakati''.

Nyota huyo alikiri kwamba matamshi yake ambayo yanafananishwa na mauaji ya rais Abraham Lincoln yaliotekelezwa na muigizaji John Wilkes Booth 1865 yatazua hisia.

''Najua hii itakuwa katika vyombo vya habari na itatisha'',alisema.

''Ni swali tu, sikati tamaa ya mtu yeyote''.

Muigizaji huyo sio wa kwanza kusema kuhusu kumuua rais.