Baadhi ya Watanzania wapinga kauli ya Magufuli kuhusu watoto wa shule wajawazito
Huwezi kusikiliza tena

Baadhi ya Watanzania wapinga kauli ya Magufuli kuhusu watoto wa shule wajawazito

Kauli ya Rais wa Tanzania John Magufuli kwamba wasichana wanafunzi wanaopata ujauzito wasirudi shuleni imepingwa na baadhi ya wananchi na wanaharakati wakisema wasichana hawa wana haki ya kikatiba kuendelea na elimu.

Siku ya Alhamisi Rais Magufuli alitoa msimamo kwamba uongozi wake hautaruhusu wanafunzi hawa warudi shuleni wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Chalinze, pembeni kidogo mwa Dar es Salaam.

Sammy Awami ana taarifa zaidi