Shirika la ndege lakatazwa kutowabadilishia viti wanawake Israel

Shirika la ndege lakatazwa kutowabadilishia viti wanawake Israel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shirika la ndege lakatazwa kutowabadilishia viti wanawake Israel

Shirika la ndege la Israel EI AI limepigwa marufuku kutowaomba wanawake kubadilisha viti iwapo mwanamume wa kiyahudi atakataa kukaa karibu nao ,mahakama imeamuru.

Abiria Renee Rabinowitz ambaye ana umri wa miaka 80 aliwasilisha kesi dhidi ya shirika hilo la ndege baada ya kutakiwa kuondoka katika kiti ambacho angekaa na mwanamume wa kiyahudi.

Jaji wa Jerusalem alisema kuwa maombi kama hayo ni ya kibaguzi.

Hatahivyo shirika hilo la ndege linasema kuwa haliwalazimishi abiria kubadilishana viti.

Bi Rabinowitz ambaye ni manusura wa Holocaust alikuwa akisafiri kutoka Newark nchini Marekani kuelekea Tel Aviv 2015 wakati alipoombwa na mfanyikazi mmoja wa ndege kubadilisha kiti.

Alisema alihisi kuaibishwa.

Wanaume walio na msimamo mkali kuhusu dini na utamaduni nchini humo hujaribi kujizuia kuwagusa wanawake isipokuwa wake zao pekee ili kutovutiwa na uhusiano wa ziada.

Makundi ya kupigania haki za kibinaadamu nchini Israel ambayo yalikuwa yakimwakilisha bi Rabinowitz katika kesi hiyo walisema kuwa ushindi huo ulikuwa mkubwa katika vita virefu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia.