Trump: Mgogoro wa mashariki ya kati ni swala la kifamilia

Rais Donald Trump amesema kuwa mzozo unaoendelea kati ya mataifa ya mashariki ya kati ni wa kifamilia
Image caption Rais Donald Trump amesema kuwa mzozo unaoendelea kati ya mataifa ya mashariki ya kati ni wa kifamilia

Marekani inasema mzozo unaoendelea kwenye mataifa ya Ghuba kati ya Qatar na majirani wake ikiwemo Saudia na milki za kiarabu, si jambo la kuchukuliwa kwa uzito.

Ikulu ya White House imeeleza mzozo huo kuwa ni mvutano wa kifamilia ambao unafaa kusuluhishwa na mataifa yanayozozana.

Saudi Arabia na washirika wake wanaishtumu Qatar kuwa inaunga mkono magaidi, na wametoa orodha ya madai yakiwemo, kuitaka Qatar kukatiza uhusiano na Iran na kufunga kituo cha habari cha Aljazeera.

Qatar inasema madai hayo hayana msingi wowote.

Mada zinazohusiana