Tetesi za soka Ulaya Jumamosi na Salim Kikeke

Arsenal waanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji Alexander Lacazette kutoka Lyon Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal waanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji Alexander Lacazette kutoka Lyon

Arsenal wamekuwa na mazungumzo zaidi na Lyon kuhusu mshambuliaji Alexander Lacazette, 26, ambaye huenda akasajiliwa kwa kuvunja rekodi ya Arsenal, kwa pauni milioni 49 (Telegraph).

Arsenal wanajiandaa kulipa euro milioni 60 ili kumsajili Alexandre Lacazette kutoka Lyon. Lacazette alikuwa anakaribia kuhamia Atletico Madrid kabla ya timu hiyo kufungiwa kusajili (L'Equipe).

Chelsea wamekubaliana kimsingi na Monaco kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, na wana matumaini ya kukamilisha uhamisho huo wa pauni milioni 35.1 wiki ijayo (Evening Standard).

Manchester United wanapiga hatua katika kumfuatilia mashambuliaji Alvaro Morata, 24, lakini bado hawajakubaliana ada ya uhamisho na Real Madrid (ESPN).

Liverpool watapanda dau jingine kumtaka Kylian Mbappe, 18, ikiwa wanaamini kuwa kweli mshambuliaji huyo anataka kuhamia Uingereza (Times).

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amezungumza na Kylian Mbappe na kujadili uhamisho wake kwenda Emirates na pia mipango ya mbele ya uchezaji wake (L'Equipe).

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amemuambia Kylian Mbappe kuwa atauza mmoja wa washambuliaji wake ikiwa mchezaji huyo atakubali kuhamia kwa mabingwa hao wa Ulaya (L'Equipe).

Arsenal wapo tayari kumuuza Alex Oxlade-Chamberlain, 23, huku Liverpool wakimtaka mchezaji huyo, ambaye huenda akawa miongoni mwa wachezaji saba watakaouzwa na Arsenal msimu huu (Independent).

Newcastle wanakaribia kukamilisha mkataba wa pauni milioni 8.7 kumsajili beki wa Eibar, Florian Lejuene 26 (Evening Chronicle).

Bayern Munich wanataka kumsajili winga wa Atletivo Madrid Yannick Carrasco, 23, ambaye anauzwa kwa pauni milioni 43 (AS).

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 31, anashindwa kupata klabu ya kwenda kwa kuwa timu nyingi hazipo tayari kulipa mshahara wake mkubwa pamoja na ada ya uhamisho (Mirror).

Manchester United wametupilia mbali tetesi kuwa Nemanja Matic amefikia makubaliano ya maslahi binafsi kuhamia Old Trafford (Daily Telegraph).

Manchester United wametoa dau la euro milioni 70 kumtaka beki wa Paris Saint-Germain Marquinhos (Globo Esporte).

Ousmane Dembele anataka kuondoka Borussia Dortmund kufuatia kufukuzwa kazi kwa meneja Thomas Tuchel. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa hataki kwenda Barcelona, lakini Chelsea na Manchester United zinamfuatilia (Eurosport).

Stoke City wameionya Arsenal kutomfuatilia kipa wake Jack Butland, 24 (Stoke Sentinel).

Manchester City wanasisitiza kuweka kipengele cha kumnunua tena Kelechi Iheanacho, 20, kwenye mkataba wake wa mauzo, huku Leicester City na West ham wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria (Telegraph).

Manchester United wanamtaka beki wa kushoto wa Barcelona Jordi Alba, 28, lakini itakuwa vigumu kumpata msimu huu (ESPN).

Winga wa Everton Gerard Deulofeu, 23, anasakwa na Roma (Romanews).

Huddersfield, waliopanda daraja msimu huu EPL, wanajiandaa kulipa pauni milioni 11.5 kumsajili mshambuliaji wa Montpellier Steve Mounie 22 (Mirror).

Galatasaray wamepanda dau la kumtaka kiungo wa Chelsea Mario Pasalic, 22, ambaye alihamia darajani mwaka 2014 lakini hajawahi kucheza (Miliyet).

Barcelona wana matumaini kuwa huenda wakafikia makubaliano ya kumsajili Ousmane Dembele, 20, kutoka Borussia Dortmund msimu ujao (Mundo).

Brighton watamfuatilia kiungo wa Middlesbrough Stewart Downing, 32, ambaye ameambiwa na meneja wake Garry Monk kuwa anaweza kuondoka Riverside (Sun).

Manchester United wamepata matumaini ya kuweza kumsajili Renato Sanches kutoka Bayern Munich, baada ya timu hiyo ya Ujerumani kumsajili Corentin Tolisso (The Sun).

Tottenham wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 17.5 kumsajili kiungo wa Schalke Max Meyer (The Sun)

Bayern Munich sasa wanaelekeza juhudi zao kumsajili Yannick Ferreira Carrasco, baada ya kupunguza kasi ya kutaka kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal (L'Equipe).

Chelsea wanakaribia kumsajili beki wa kati wa Southampton Virgil va Dijk kwa pauni milioni 60 (Sky Italia).

Kiungo wa Monaco Fabinho, 23, atagharimu euro milioni 45. Juventus, Manchester United, Manchester City na Paris Saint-Germain wanamtaka mchezaji huyo kutoka Brazil (Calcio Mercato).

Manchester United wanamnyatia beki wa Barcelona Jordi Alba (ESPN).

Dau la pauni milioni 31 la Manchester United kumtaka Andre Gomes limekataliwa na Barcelona (Catalunya Radio).

Tottenham wanataka kumsajili kiungo wa AC Milan Suso (Marca).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Weekend Njema nyote!!