Mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani atajwa

Martha, ametajwa kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Martha, ametajwa kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani.

Martha, ametajwa kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani.

Shindano la kila mwaka ambalo sasa liko katika mwaka wake wa 29 lilifanyika katika eneo la Petalum mjini Carlifornia.

Martha anayemilikiwa na Shirly Zindler aliwashinda wapinzani 13 na kupewa taji na pesa taslimu dola 1,500.

Mbwa huyo mwenye taya kubwa sasa atasafirishwa hadi mjini New York kwa maonyesho ya vyombo vya habari kulingana na waandalizi wa shindano hilo.

Maonyesho hayo ya Sonoma Marin yanasema kuwa shindano hilo huwashirikisha mbwa wengi ambao wameokolewa katika makaazi na maeneo ya kukuza mbwa kwa lengo la kuwauza.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani

Martha ni mbwa aliyeokolewa ambaye karibia awe kipofu kutokana na kupuuziliwa mbali alisema bi Zindler.

''Baada ya kufanyiwa upasuaji sasa anaweza kuona tena na hahisi uchungu wowote''.

Shirika la habari la AP limesema kua Martha aliibuka mshindi kwa kutembea katika ukumbi na kuwavutia majaji.

Majaji hao walimpatia ushindi mbwa huyo kutokana na hisia za watu, sura, tabia na hisia zake.