Marekani yaondoa zawadi ya $5m kwa aliyekuwa kiongozi wa Alshabab

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab
Image caption Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeghairi kutoa zawadi ya mpaka dola milioni tano kwa aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Shabab.

Haijatoa sababu ya uamuzi wake wa kumtoa Mukhtar Robow kwenye orodha ya tuzo za haki.

Bw Robow bado anachukuliwa kama gaidi na Idara ya Hazina ya Marekani.

Alikuwa kamanda wa jeshi, kiongozi wa kidini na msemaji wa al-Shabab, lakini baadae akakorofishana na aliyekuwa kiongozi wakati huo, Ahmed Abdi Godane, mwaka 2013.

Kuna ripoti kuwa Bw Robow anafanya mazungumzo na serikali ya Somalia lakini hilo halijathibitishwa.