Fabinho: Mwaliko wa Mourinho unaweza ''kunishawishi''

Kiungo wa kati wa Monaco Fabinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Monaco Fabinho

Uhamisho wa kuelekea Manchester United unaweza ''kunishawishi'' amesema kiungo wa kati wa Monaco Fabinho ambaye amehusishwa na klabu hiyo ya Old Trafford.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alifunga mabao 11 katika mechi 50 katika mashindano yote msimu uliopita huku timu yake ikishinda taji la ligi.

United tayari imemsajili beki Victor Lindelof katika kikosi chao huku wakijaribu kuimarisha mchezo wao ili kupanda katika jedwali la ligi ya Uingereza kutoka nafasi ya sita.

''Manchester United ni tmu kubwa na nitafikiria kuhusu wazo hilo'', alisema fabinho.

''Iwapo Mkufunzi wa Manchester United atanialika basi mwaliko wake utakuwa na ushawishi mkubwa'', aliambia runinga ya Esportivo Interativo.

Lakini nitalazimika kuzungumza na ajenti wangu na Monaco ili kufanikisha hatua hiyo.