Yemen inakabiliwa mlipuko mbaya wa kipindupindu

Hakuna sehemu nchini Yemen ambayo haijaathirika na ugonjwa wa kipindupindu Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hakuna sehemu nchini Yemen ambayo haijaathirika na ugonjwa wa kipindupindu

Shirika la Afya Duniani WHO na lile la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto-UNICEF, yanasema kuwa, taifa la Yemen kwa sasa linakabiliwa na mlipuko mmbaya sana wa ugonjwa wa kipindupindu, kuwahi kushuhudiwa duniani.

Kwa mjibu wa Umoja wa Mataifa, kuna zaidi ya visa laki mbili za ugonjwa huo nchini humo.

Zaidi ya watu elfu 13 wamefariki kufikia sasa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watoto ndio walioathirika pakubwa na kipindupindu

Kuenea kwa ugonjwa huo, kumetokana na kuporomoka kwa huduma za afya, baada ya muda mrefu wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen.

Umoja wa mataifa sasa unatoa wito kwa mamlaka ya nchi hiyo, kuwalipa wafanyikazi wa afya wapatao elfu 30, mafao yao, baada ya kukaa bila mshahara kwa miezi 10 sasa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hospitali zimelemewa na idadi kubwa ya wanaougua ugonjwa wa kipindupindu