Rais Sisi aidhinisha kusalimishwa visiwa kwa Saudi Arabia

File photo taken on 14 January through the window of an airplane shows the islands of Tiran (foreground) and Sanafir (background) in the Red Sea Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Sisi aidhinisha kusalimishwa visiwa kwa Saudi Arabia

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi, ameidhinisha mkataba ya umiliki wa visiwa viwili vilivyoko katika maeneo ya bahari ya Sham, kwa Saudi Arabia.

Wakili wa serikali Rafiq Sharif, amesema kuwa amri hiyo ya Rais Sisi, imekuwa sheria na kwa sasa visiwa hivyo vitakuwa ni mali ya Saudi Arabia.

Lakini bado mahakama ya kikatiba inafaa kutoa agizo lake la mwisho, ambapo taasisi hiyo ya kisheria na Bunge la nchi hiyo, ndio yaliyo na uwezo wa kutoa agizo la mwisho.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hatua ya kuachia Saudi Arabia visiwa hivyo, vilisababisha maandamano na pingamizi kubwa kutoka kwa raia nchini Misri,

Muafaka huo, umekuwa ukipingwa na kuzuiwa kufanya kazi katika vuta ni kuvute iliyokuwepo, kwa mwaka mzima nchini Misri.

Hatua ya kuachia Saudi Arabia visiwa hivyo, vilisababisha maandamano na pingamizi kubwa kutoka kwa raia nchini Misri, pale agizo hilo lilipotangazwa mwaka jana na Rais al Sisi.

Mwaandishi wa BBC mjini Cairo, anasema kuwa ikiwa Misri haitokubalia kuachia Saudi Arabia visiwa hivyo, bila shaka huenda wakanyimwa fedha nyingi za uwekezaji kutoka kwa taifa hilo la kiarabu, lenye uchumi mkubwa.

Image caption Visiwa