Ndege iliyokuwa ikitingishika yalazimika kutua Australia

Huwezi kusikiliza tena
Watch: Passenger films on board the flight

Ndege moja ya shirika la AirAsia iliyokuwa safarini kueleka mjini Kuala Lumpur, imelazimika kurudi nchini Australia kufuatia hitilafu ya mitambo ambayo ilisababisha ndege hiyo "kutingishika kama mashine ya kuoshea."

Rubani wa ndege hiyo alisema kuwa uamuzi wa kurudisha ndege hiyo mjini Perth dakika 90 baada ya kuondoka uliochukuliwa kufuatia hitilafu ya kimitambo.

Ndege hiyo ilirudi na kutua salama mapema Jumapili.

Polisi walisema watoa huduma za dharura za baharini mjini Perth, waliweka katika hali ta tahadhari kujiandaa iwapo ndege hiyo ingetua baharini.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege ya AirAsia

Abiria kadha waliokuwa ndani ya ndege hiyo walisema kuwa ndege hiyo ilipatwa na hitilafu ya injini hali iliyosabisha itingike.

AirAsia bado haijazungumzia tukio hilo na hakuna majeraha yaliyoripitiwa.

Mapema mwezi huu ndege ya Airbus A330 ya shirika la China Eastern Airlines, ilizazimika kutua ghafla baada ya shimo kubwa kutokea moja ya injini zake.