Pandekezo la Korea Kaskazini na Kusini kushiriki mashindano pamoja

Pandekezo la Korea Kaskazini na Kusini kushiriki mashindano pamoja
Image caption Pandekezo la Korea Kaskazini na Kusini kushiriki mashindano pamoja

Rais wa Korea Kusini amependekezaa kuwa nchi yake na ile ya Korea Kaskazini zibuni kikosi cha pamoja kitakachoshiriki katika mashindano ya msimu wa baridi mwaka 2018.

Moon Jae-in anasema ana matumaini ya kurudi nyakati ambapo nchi hizo mbili zilitoa kikosi cha pamoja katika mashindano ya kimataifa na kutembea pamoja katika shere za olimpiki.

Korea Kaskazini bado haijathibitisha ikiwa itatuma kikosi chake kwenye mashindano ya msimu wa baridi ambayo yataandaliwa na Korea Kusini katika mji wa Pyeopngchang.

Bwana Moon pia amependeza kuwa Korea Kaskazini na Kusini ambazo zina migogoro mikali ziwasilishe ombi la pamoja kuandaa kombe la dunia mwaka 2030.