Kura ya maoni yasitishwa Mali

Kumekuwa na mapigano makali Kaskazini mwa Mali kati ya wa Mali
Image caption Kumekuwa na mapigano makali Kaskazini mwa Mali kati ya wa Mali

Vugu vugu maarufu la kisiasa nchini Mali, limetoa wito wa kusitishwa kwa kura ya maoni itakayotoa fursa ya kufanyia marekebisho katiba ya taifa hilo hadi pale serikali itakapotwaa udhibiti wa maeneo yake yote.

Vugu vugu hilo linalojiita "Don't touch my Constitution"ama usiguse katiba yangu, pia linataka kufanywe mashauriano ya kitaifa kabla ya kuidhinishwa kwa mabadiliko yanayopendekezwa.

Image caption Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana kutaka katiba mpya

Kura hiyo iliyoahirishwa wiki iliyopita inapania kujumuishwa kwa mkataba wa amani uliyofikiwa mwaka 2015, kati ya serikali na makundi yaliyojitenga, kukomesha mapigano Kaskazini mwa Mali.

Hata hivyo mapigano katika eneo hilo yamekuwa yakiendelea huku makundi yenye itikadi kadi kali za kidini yakifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya vikosi vya serikali na walinda amani wa kimataifa.