Wapiganaji wa IS washambulia Iraq

Shambulizi hilo linatajwa kama kisasi kwa serikali ya Iraq
Image caption Shambulizi hilo linatajwa kama kisasi kwa serikali ya Iraq

Ripoti kutoka mji wa Mosul, nchini Iraq zinaarifu kuwa, wapiganaji wa Islamic State wamefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika wilaya za magharibi ya mji huo wa kale.

Wapiganaji hao wa IS wameshambulia raia na kuchoma moto nyumba na magari katika wilaya mbili ambayo majeshi ya serikali yalifanikiwa kukomboa kutoka mikononi mwao hivi karibuni.

Jeshi la Iraq hata hivyo linasema kuwa limefanikiwa kuzima mashambulio kubwa IS.

Awali jeshi hilo lilisema kuwa limekomboa karibu maeneo yote ya mji wa kale wa Mosul ambayo ni ngome kuu ya wapiganaji wa Islamic State.