Mitandao ya Ohio yadukuliwa na ujumbe wa IS kuchapishwa

Web hack
Image caption Mitandao ya Ohio yadukuliwa na ujumbe wa IS kuchapishwa

Mitandao kadha ya serikali katika jimbo la Ohio nchini Marekani ukiwemo wa Governor John Kasich imedukuliwa na ujumbe wa kuunga mkono kundi la Islamic State kuchapishwa.

Ujumbe huo ulisema , Donald Trump atawajibika kwa kila tone la damu linalomwagika kwenye nchi za kiislamu na kumalizia kusema "Nunaipenda Islamic Stete".

Udukuzi huo ulifanywa na kundi linalojiita Team System DZ.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtandao wa Gavana John Kasich ulidukuliwa

Mtandao wa gavana wa jimbo la Ohio ulikuwa bado huajarekebishwa

Ujumbe kwenye mtandao ulikuwa na ishara ya kiarabu na ulikuwa maandishi meusi na meupe ambayo hutumiwa kwenyew bendera ya Islamic State.

Ujumbe kwenye mtandao wa Bwana Kasich ulicheza wimbo wa kuitisha maombi ya kiislamu.

Image caption Mitandao ya Ohio yadukuliwa na ujumbe wa IS kuchapishwa

Mada zinazohusiana