Manowari ya Uingereza kuanza kufanyiwa majaribio leo

HMS Queen Elizabeth ndiyo meli kubwa zaidi kuwai kuundwa kwa jeshi la wanamaji la Uingereza Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption HMS Queen Elizabeth ndiyo meli kubwa zaidi kuwai kuundwa kwa jeshi la wanamaji la Uingereza

Manowari mpya ya Uingereza inatarajwa kuanza majaribio ya baharini leo.

HMS Queen Elizabeth ndiyo meli kubwa zaidi kuwai kuundwa kwa jeshi la wanamaji la Uingereza iliwa na uwanja wa ndege wenye ukubwa wa viwanja vitatu vya soka.

Meli hiyo ni kubwa hadi itahitaji kusubiri kushuka kwa viwango vya maji kuweza kupititia eneo la Forth bridges.

Mashua zingine zitahitaji kuisindikiza meli hiyo kutoka ilikotia nanga huko Scotland.

Hata hivyo itachukua miaka kabla kabla ya manowari ya HMS Queen Elizabeth kuanza kutumiwa na kubeba ndege.

Mada zinazohusiana