Je wamkumbuka vipi mcheza soka El Hadji Diouf?

El Hadji Diouf
Image caption Je wamkumbuka vipi mchezaji El Hadji Diouf?

Wakati ya kipindi cha taaluma yake ya usakataji soka, El Hadji Diouf alipata sifa ya kijana mtukutu wa kandanda.

Sasas akiwa amestaafu, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal anasema kuwa sifa ya kijana mtukutu wa kandanda haukuwa hakuwa nzuri.

El Hadji Diouf ni shujaa nchini Senegal na kila mahala anakokwenda hushangiliwa na mashabiki wakiwemo vijana na hata wazee.

Watu nchini Senegal bado wanamshukuru kwa wajibu aliotekeleza wakati wa kombe la dunia mwaka 2002 nchini Japan na Korea Kusini.

Lakini nchini Uingereza anakumbukwa kwa sarakasi zake uwanjani kuliko umahiri aliokuwa nao katika usakataji kandanda.

Ni tabia ililomfuata hadi kwa ligi za Uingereza alipocheza na Liverpool na Blackburn Rovers hadi Bolton Wanderes na Rangers ya Scotland.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kombe la dunia mwaka 2002 El Hadj Diouf (kati kati)

Diouf aliwatemea mate wapinzani na kuwakabili wasimamizi wa mechi na wapinzani.

Lakini sasa akiwa amestaafu anaeleza historia.

Mimi ni simba, nina tabia hiyo na ninataka watu wanisheshimu.

Diouf ambaye sasa amehamia mji mkuu wa Senegal Dakar, anasema kwa mara kadha hakueleweka vyema wakati wa siku zake akicheza England.

Hata hivyo anakiri amefanya mambo mabaya.

Alipoulizwa na mambo yapi, alisema alikuwa akiwatemea mate wapinzani labda walipomuambia kitu ambacho hakukipenda.

Haki miliki ya picha El Hadji Diouf
Image caption Rais Macky Sall na El Hadji Diouf

Mada zinazohusiana