Waliomuingiza mtu mweusi kwenye jeneza mahakamani Afrika Kusini

Willem Oosthuizen na Theo Jackson
Image caption Willem Oosthuizen na Theo Jackson

Wakulima wawili weupe watafikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini , baada ya kutuhumiwa kuwa walimsukuma mtu mmoja mweusi na kumuingiza ndani ya jeneza, huku wakitishia kumwagia mafuta ya petroli na kumteketeza moto, akiwa hai.

Wakati Victor Mlotshwa alipokataa, wakulima hao walimtishia kuwa watamweka ndani ya jeneza hilo pamoja na nyoka.

Haki miliki ya picha youtube
Image caption Wakati Victor Mlotshwa alipokataa, wakulima hao walimtishia kuwa watamweka ndani ya jeneza hilo pamoja na nyoka.

Washtakiwa hao Willem Oosthuizen na Theo Jackson, walikamatwa mwezi Novemba mwaka jana, baada ya video ya kitendo hicho kilipowekwa mitandaoni.

Walisema kuwa, Bwana Mlotshwa alipitia kwenye shamba lao liliko katika jimbo la Mpumalanga, bila ya kuwa na idhini, na walikuwa wakimuadhibu.

Katika kusikizwa kwa kesi hiyo awali, jaji wa mahakama alisema kuwa wakulima hao walikuwa wakatili na waliojaa tabia za ubaguzi wa rangi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Victor Mlotshwa

Mada zinazohusiana