China yamuachilia mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mgonjwa wa saratani

Chinese dissident Liu Xiaobo is seen in this undated photo released by his families. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Liu Xiaobo alifungwa jela mwaka 2009 kwa mashtaka ya kutaka kuwepo demokrasia zaidi.

Mshindi wa tuzo la amani la Nobel Liu Xiaobo ameachiliwa kutoka gerezani baada ya kupatwa akiwa na saratani ya ini.

Bwana Liu ambaye ni mpiganiaji wa haki za binadamu alifungwa jela mwaka 2009 kwa mashtaka ya kutaka kuwepo demokrasia zaidi.

Wakili wake anasema kuwa anatibiwa hospitalini mkoa wa Liaoning baada ya kupatikana na ugonjwa huo mwezi uliopita.

Mkewe Liu Xia amekuwa kwenye kifungo cha nyumbani tangu mumewe ashinde tuzo la amani la Nobel mwaka 2010 na hajawai kufunguliwa mashtaka.

Liu Xiaobo mwenye umri wa miaka 61 alikuwa kiongozi mkuu kwenye maandamano ya Tiananmen Square mwaka 1989.

Utawala wa China haujasema ni kwa nini umemzuilia mkewe.

Hakuenda kupewa tuzo lake na aliwakilishwa na kiti. Serikali ya China inamtaja kuwa mhalifu na ilighadhabishwa na tuzo hilo.

Uhisiano na Norway ulikatwa na kurejeshwa Disemba.