Tabiti zinaweza kuchukua nafasi ya walimu Tanzania?

Tabiti zinaweza kuchukua nafasi ya walimu Tanzania?

Watoto takriban 250 milioni kote dunia huwa hawawezi kusoma na kuandika na pia hawana ujuzi wa kufanya hesabu.

Wengi huwa katika nchi zinazoendelea ambapo huwa vigumu kuwapata walimu wazuri.

Global Learning XPrize ni shindano ambalo linashirikisha makundi ya wataalamu maeneo mbalimbali duniani kuunda programu tumishi za kutumiwa katika tabiti (tablet) ambazo zinaweza kuwasaidia watoto kusoma.

Wiki hii, timu 11 zilichaguliwa kutoka kwa timu 200.

Timu zilizofaulu zitaingia katika awamu inayofuata ya shindano hilo.

Kila timu inahitajika kuunda programu ambayo inawawezesha watoto husoma wenyewe bila usaidizi wa mtu mwingine.

Mwandishi wa BBC Dan Simmons alitembelea moja ya vijiji 150 kaskazini mwa Tanzania ambavyo vinashirikishwa katika kufanyia majaribio programu tumishi kadha kwenye tabiti.