Venezuela kuelekea katika utawala wa kijeshi?

Rais Nicholas Maduru amekua akidaiwa kutumia nguvu kukabiliana na maandamano
Image caption Rais Nicholas Maduru amekua akidaiwa kutumia nguvu kukabiliana na maandamano

Muendesha mashtaka mmoja wa ngazi ya juu nchini Venezuela amesema taifa hilo linaelekea kuwa na na utawala wa kijeshi ambapo idara ya mahakama haina uwezo wa kuwachukulia hatua maafisa wanaokiuka sheria.

Katika mahojiano na na gazeti moja la Peru(El Comercio) Luisa Ortega Diaz amesema visa vya wanajeshi kukiuka haki za binadamu vimeongezaka katika siku za hivi karibuni.

Zaidi ya watu sabini wameuawa tangu mwanzo wa mwezi wa nne mwaka huu.

Bi Ortega ni mmoja wa maafisa wachache wa serikali kumshutumu Rais Nicholas Maduru.