Rais wa Brazil ashitakiwa kwa ufisadi

Michel Temer aliingia madarakani mwaka 2016 kuchukua nafasi ya Dilma Rousseff ambaye pia aliondolewa kwa ufisadi
Image caption Michel Temer aliingia madarakani mwaka 2016 kuchukua nafasi ya Dilma Rousseff ambaye pia aliondolewa kwa ufisadi

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Brazil, amemhukumu Rais Michel Temer kwa kosa la kupokea hongo, mojawapo ya kosa la kwanza kati ya misururu kadhaa ya makosa chungu nzima ya ufisadi yanayomuandamana kingozi huyo aliyeko mashakani.

Temer amekatalia mbali wito unaotolewa wa kujiuzulu kuhusiana na makosa hayo, huku akisema kuwa hana hatia yoyote.

Mahakama kuu nchini Brazil sasa ndio itakayoamua, ikiwa kesi hiyo itaendelea na kuwasilishwa katika Bunge la uwakilishi, ili kupigiwa kura ya kumuondolea mashtaka Temer au la.