Trump aitaka mahakama kulinda usalama wa Marekani

Trump anapingwa vikali na wanaharakati kwa kupinga raia wa baadhi ya nchi za kiislam kuingia Marekani
Image caption Trump anapingwa vikali na wanaharakati kwa kupinga raia wa baadhi ya nchi za kiislam kuingia Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani, amesema kuwa, agizo la Mahakama kuu nchini humo la kukabaliana na marufuku aliyoitoa yenye utata ya kuwazuia baadhi ya watu kusafiri hadi Marekani kuanza kufanya kazi, ni hatua kubwa kwa usalama wa taifa hilo.

Idara ya mahakama inasema kwamba, marufuku hiyo inaweza kukubaliwa japo kwa kiasi fulani, kwa wasafiri wasio na uhusiano wa moja kwa moja kwa watu au maeneo nchini Marekani huku ikisubiri uamuzi wa mwisho.

Hilo linafaa kuanza kufanya kazi mwezi Oktoba mwaka huu.

Mojawapo ya sera za Trump wakati akigombea kuingia madarakani ilikuwa ni kuzuia raia wa baadhi ya nchi za kiislam kuingia Mrekani.